Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:54

UN yaonya kuhusu athari za joto lililokithiri duniani


Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Antonio Guterres.

Umoja wa mataifa ulionya Jumanne kwamba Ulimwengu unapaswa kuwa tayari kukabiliana na mawimbi, ya joto kali, linalozidi  kuongezeka, wakati mataifa ya ukanda wa kaskazini, yakikabiliwa na hali ya joto iliyokithiri.

"Matukio haya yataendelea kuongezeka kwa kasi, na dunia inahitaji kujiandaa kwa mawimbi makali zaidi ya joto," John Nairn, mshauri mkuu wa hali ya hewa kali, katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO), aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswizi.

Kauli yake ilikuja wakati Ulaya ikikabiliana na ongezeko la joto siku ya Jumanne, na moto wa msituni ambao umeteketeza maeneo mengi ya ukanda wa Kaskazini, na kulazimisha kuhamishwa kwa watoto 1,200, karibu na eneo la mapumziko lilo lwenye ufukwe wa bahari nchini Ugiriki.

Mamlaka za afya zimetoa tahadhari kutoka Amerika ya Kaskazini hadi Ulaya, na Asia, zikiwataka watu kuhakikisha wana maji ya kunywa na kujikinga na jua kali, hali ambayo inaashiria athari za ongezeko la joto duniani.

Mawimbi ya joto ni miongoni mwa hatari kubwa zaidi za asili, huku mamia ya maelfu ya watu wakifa kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika, zinazohusiana na joto kila mwaka, Nairn alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG