Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:53

Guterres apeleka barua kwa Putin juu ya pendekezo la kukidhi mahitaji ya wote


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. June 19, 2023. New York. (Photo by Yuki IWAMURA / AFP)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. June 19, 2023. New York. (Photo by Yuki IWAMURA / AFP)

Mpango ambao unaruhusu usafirishaji nje wa nafaka za Ukraine kutoka bandari ambazo Russia imezifunga wakati wa uvamizi wake kwa Ukraine hapo mwaka jana, unatakiwa kuhakikiwa ifikapo Julai 18

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempelekea barua Rais wa Russia Vladimir Putin, akielezea pendekezo linalolenga kukidhi matakwa ya Russia ambayo yanatishia kufunga mpango muhimu wa nafaka katika Black Sea Grain Initiative.

“Katibu mkuu bado anashirikiana na pande zote husika katika suala hili na anaonyesha nia yake ya kuendelea na pendekezo lake na Russia”, msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano.

Dujarric alikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu pendekezo hilo, akisema “tuko katika nyakati ngumu sana.” Mpango huo ambao unaruhusu usafirishaji nje wa nafaka za Ukraine kutoka bandari ambazo Russia imezifunga wakati wa uvamizi wake kwa Ukraine hapo mwaka jana, unatakiwa kuhakikiwa ifikapo Julai 18.

Moscow imesema mara kwa mara katika kipindi cha kuelekea tarehe za mwisho za uhakiki uliopita, kwamba haifaidiki vya kutosha chini ya mpango huo na imetuma ishara kama hizo hivi karibuni. Mkataba wa maelewano kati ya Moscow na Umoja wa Mataifa umetaka kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa nafaka na mbolea kutoka Russia.

Wakati chakula na mbolea havijawekewa vikwazo na nchi za Magharibi, juhudi zimefanywa ili kupunguza hofu kwa mabenki yenye wasiwasi, bima, meli na watendaji wengine wa sekta binafsi kuhusu kufanya biashara na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG