Tofauti katika masuala "ikiwa ni pamoja na waasi kuhamia katika nyumba za raia katika mji mkuu na vituo vya umma, hospitali na barabara" yamesababisha ukosefu wa makubaliano kumaliza uhasama, jeshi lilisema.
Mapigano yalizuka mwezi Aprili, wakati jeshi na kikosi maalum cha Msaada wa dharura (RSF) wakigombea madaraka. Tangu wakati huo, zaidi ya watu milioni tatu wameondolewa katiia makazi yao, wakiwemo zaidi ya watu 700,000 ambao wamekimbilia nchi jirani.
Katika mapigano hayo watu takriban 1,136 wameuawa, kulingana na wizara ya afya, ingawa maafisa wanaamini idadi huenda ikawa kubwa zaidi.
Wakati pande mbili zinazopigana zimeonyesha uwazi wa kutaka juhudi za upatanishi zinazoongozwa na watendaji wa kikanda na kimataifa, hakuna matokeo yoyote katika juhudi zinzoendelea za kusitisha mapigano.
Pande hizo mbili zilianza tena mazungumzo, yanayosimamiwa na Saudi Arabia pamoja na Marekani, mjini Jeddah mwezi huu.
Chanzo cha habari hii nia shirika la habari la Reuters
Forum