Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 10:12

Zaidi ya mataifa 40 yakutana Saudi Arabia kujadili kurejesha amani Ukraine


Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman akiwa na viongozi kwenye mkutano wa C5 mwezi uliopia. Picha ya maktaba.
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman akiwa na viongozi kwenye mkutano wa C5 mwezi uliopia. Picha ya maktaba.

Waangalizi wamesema Jumapili kwamba Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa mkutano unaolenga kutatua mzozo wa Ukraine kwa amani kunaashiria kuendelea kuimarika kwa ushawishi wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta kwenye jukwaa la kimataifa.

Taifa hilo limeleta pamoja takriban mataifa 40 yenye misimamo tofauti yakiwemo Marekani, China na India pamoja na mengine kutoka upande wa kusini, ili kujadili mzozo huo. Katika siku ya pili ya kikao hicho mjini Jeddah, mazungumzo yalikuwa yakiendelea baina ya mataifa hayo wakati maafisa wakuu kutoka Ukraine pamoja na washirika wake kutoka magharibi kama vile Marekani na Umoja wa Ulaya wakihudhuria, na pia mataifa kutoka upande ya Kusini mwa ulimwengu, ambayo baadhi yamekuwa hayaegemei upande wowote au baadhi yakiwa washirika wa Russia kwenye mzozo huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa China kushiriki mazungumzo ya aina hiyo, ingawa Beijing imedumisha ushirikiano wa karibu wa kiuchumi na kidiplomasia na Russia, na kukataa kukemea Moscow wazi wazi kutokana na uvamizi wake. Hata hivyo Russia haijahudhiria kikao hicho lakini inasemekana kufuatilia kwa kina mazungumzo yanayoendelea. Waangalizi pamoja na maafisa wa magharibi wanasema kwamba Saudi Arabia imekuwa muhimu katika kushawishi China kuhudhuria mazungumzo hayo. Maafisa wa Saudi Arabia wanayaona mazungumzo hayo kama hatua muhimu katika kuimarisha sera ya ushirikiano dhabiti na Ukraine, China na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG