Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 07:51

Mkutano wa kimataifa wa kupambana na ufisadi waanza mjini Washington


Picha iliyopigwa kutoka angani jioni June 15, 2014 ikionyesha mandhari ya Jiji la Washington, DC, ikiwa ni pamoja na jengo la Lincoln Memorial, Mnara wa Washington Monument, Bunge la Marekani US na eneo la National Mall.
Picha iliyopigwa kutoka angani jioni June 15, 2014 ikionyesha mandhari ya Jiji la Washington, DC, ikiwa ni pamoja na jengo la Lincoln Memorial, Mnara wa Washington Monument, Bunge la Marekani US na eneo la National Mall.

Mamia ya wanaharakati, maafisa na wataalam wamekusanyika mjini Washington kutafuta njia za kukomesha ufisadi katika serikali, taasisi na mifumo mbalimbali duniani.

Mamia ya wanaharakati, maafisa na wataalam wamekusanyika mjini Washington kutafuta njia za kukomesha ufisadi katika serikali, taasisi na mifumo mbalimbali duniani.

Kongamano la siku tano, ambalo huandaliwa kila baada ya miaka miwili na taasisi ya Transparency International kuangazia ufisadi duniani na nchi mwenyeji wa mkutano huo, ambapo inakadiriwa kikao hicho ni kikubwa kabisa cha kimataifa kuhusu vita dhidi ya ufisadi.

Mkutano wa Kimataifa wa Vita Dhidi ya Ufisadi (IACC) unaofanyika wiki hii unaangazia mada saba, ikiwemo usalama wa kimataifa, ukabila na mabadiliko ya hali ya hewa, masoko ya magendo na mitandao ya kihalifu, ufisadi na utakatishaji fedha, na usalama wa wanaharakati wanaopambana na rushwa.

Mkutano huo unafanyika wakati kumekuwa na ongezeko la wasiwasi juu ya kushindwa kwa serikali nyingi kutekeleza ahadi zao za kupambana na ufisadi, waandaaji wa mkutano wamesema.

“Ufisadi unaendelea kuchochea vitisho vyetu vya kimataifa na kuzuia mafanikio yanayohitajika ya utatuzi wa hivi sasa na siku za usoni ambao tutakuwa tunauangalia. Gharama yake inakadiriwa kufikia matrilioni kila mwaka,” Huguette Labelle, mwenyekiti wa Baraza la IACC, aliuambia mkutano huo katika hotuba yake ya ufunguzi.

Ufisadi unakaribisha ukosefu wa usawa na kuhamasisha ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu dunia nzima, wataalam walisema.

“Utawala mbaya unaruhusu viongozi madikteta, mafisadi na mitandao ya kihalifu iliyojipanga kuimarisha azma yao kwa kutumia mabavu na uchumi wa kimataifa, kwa gharama ya demokrasia, haki za binadamu na usalama wa kimataifa,” waandaaji wa IACC walisema katika taarifa yao ya maelezo.

Russia, China, Iran na Afghanistan ni miongoni mwa baadhi ya nchi ambazo zimetuma wawakilishi wao katika mkutano huo.

Alejandro Salas, msemaji wa Transparency International, alisema mkutano huo uko wazi kwa nchi zote, lakini baadhi ya nchi hazijaonyesha utashi wa kushiriki.

“Baadhi ya nchi zimetawaliwa, bahati mbaya, na serikali za kidikteta au ufisadi ambazo zina maslahi maalum za kuweka udhitibi mkali kwa wananchi wake kwa kunyamazisha kitu chochote kinachoonekana kama upinzani au jamii huru, uhuru wa kujieleza,” Salas aliiambia VOA.

Mshauri wa usalama wa taifa wa White House Jake Sullivan aliliambia kongamano hilo kuwa Marekani inapambana na ufisadi ndani na nje ya nchi.

FILE PHOTO: Jake Sullivan
FILE PHOTO: Jake Sullivan

“Ni lazima tuhakikishe kuwa mifumo yetu inafanya kazi ya kudadisi na siyo kusaidia tabia hizo za kifisadi,” Sullivan alisema, akiongeza kuwa sera ya Marekani kimsingi inajikita katika kuwasaidia wanaharakati wanaopambana na ufisadi, ikiwemo waandishi wa habari ambao hufichua ufisadi, na kuwafuatilia mafisadi.

Marekani na washirika wake wamekamata kiasi cha mali zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 30 zinazomilikiwa na matajiri mafisadi wa Russia, Sullivan alisema.

“Ufisadi siyo tu kuhusu viongozi madikteta wanaofanya ubadhirifu wa mali ya taifa ili kuishi kifahari. Ni kuhusu kutengeneza mfumo kamili wa utawala unaosaidiwa na washirika nje ya mipaka yao,” alisema Samantha Power, Kiongozi wa USAID.

Kwa mujibu wa kipimo cha hivi karibuni ya Ufahamu wa Ufisadi, juhudi za kupambana na ufisadi hazijapiga hatua kubwa kwa miaka kadhaa sasa, Transparency International ilisema katika ripoti yake ya mwaka iliyochapishwa.

Kipimo hicho kinaziweka nchi kulingana na ufahamu wa umma wa ufisadi katika sekta binafsi na za umma. Mwaka 2021, kipimo hicho kiliiweka Denmark, Finland na New Zealand kuwa zina ufisadi mdogo sana, na Sudan Kusini, Syria na Somalia zikiwa na ufisadi mkubwa sana kati ya serikali 180.

Kwa miaka michache iliyopita, ufahamu wa ufisadi nchini Marekani umeongezeka, ikiishusha nchi hiyo kutoka nafasi ya 16 mwaka 2017 kufikia ya 27 mwaka 2021.

XS
SM
MD
LG