Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:06

Iran: Wanawake wawili wahukumiwa kifo kwa mashtaka ya usafirishaji haramu wa binadamu


Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei

Wanawake wawili wamehukumiwa kifo nchini Iran kwa mashtaka ya “ufisadi duniani”, na usafirishaji haramu wa binadamu katika siku chache zilizopita, shirika la habari la serikali (IRNA) limeripoti Jumatatu.

Watetezi na kundi la kutetea haki walisambaza picha za wanawake hao kwenye mitandao ya kijamii, wakisema wanawake hao ambao ni wanaharakati wa haki za wapenzi ya jinsia moja hawana hatia. Shirika la habari la Reuters linasema halikuweza kuthibitisha kuhusu picha hizo.“

Kinyume na habari zilizochapishwa mtandaoni, waliohukumiwa waliwalaghai na kuwasafirisha wasichana wadogo nje ya nchi kwa kuwaahidi fursa za masomo na kazi, jambo ambalo lilipelekea waathirika kadhaa kujiua,” IRNA imesema.“

Ufisadi duniani” ni neno ambalo hutumiwa na mamlaka za Iran kumaanisha makosa mbalimbali, yakiwemo yale yanayohusiana na maadili ya kiislamu.

Mwezi Machi, kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alielezea mapenzi ya jinsia moja kama sehemu ya “upotovu wa maadili” ulioenea katika utadamaduni wa mataifa ya magharibi.

Makundi ya kutetea haki za binadamu ya nchi za magharibi yameikosoa mara nyingi Iran namna inavyoshughulikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja. Chini ya mfumo wa sheria ya Iran, vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vinaweza kuadhibiwa kwa adhabu ya kifo.

XS
SM
MD
LG