Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 22:31

Isabela do Santos bado hajaarifiwa kuhusu waranti yake kwa Interpol


Nembo ya shirika la kimataifa la polisi duniani (Interpol)
Nembo ya shirika la kimataifa la polisi duniani (Interpol)

Shirika la habari la Ureno, “Lusa” liliripoti Ijumaa kwamba Interpol ilitoa kibali baada ya waendesha mashtaka wa umma nchini Angola kulitaka shirika hilo "kumtafuta, kumkamata" na kumrejesha dos Santos

Binti bilionea wa Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, Isabel dos Santos bado hajaarifiwa kuhusu waranti ya kimataifa ya kumkamata inaoripotiwa kutolewa na shirika la kimataifa la polisi duniani (Interpol) chanzo rasmi kinachomwakilisha binti huyo kimesema Jumamosi.

Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la Reuters chanzo rasmi cha dos Santos kilisema mawakili wake "walishauriana na na Interpol na, hadi wakati huu hakuna kumbukumbu ya utoaji wa hati".

Shirika la habari la Ureno, “Lusa” liliripoti Ijumaa kwamba Interpol ilitoa kibali baada ya waendesha mashtaka wa umma nchini Angola kulitaka shirika hilo "kumtafuta, kumkamata" na kumrejesha dos Santos.

Interpol na waendesha mashtaka wa umma hawakujibu maombi ya shirika la habari la Reuters kutaka kuzungumzia suala hilo.

Ikinukuu nyaraka rasmi, Lusa ilisema mwanamke huyo mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 49 anatafutwa kwa makosa yanayomkabili ikiwa ni pamoja na ubadhirifu, udanganyifu, ushawishi na utakatishaji fedha.

Dos Santos kwa miaka mingi amekuwa akikabiliwa na tuhuma za ufisadi, ikiwemo madai ya mwaka 2020 ya Angola, kwamba wakati wa urais wa baba yake, yeye na mumewe waliingiza dola bilioni moja kama fedha za serikali kwa kampuni walizokuwa na hisa.

Mara kadhaa amekuwa akikanusha kufanya makosa yeyote.

XS
SM
MD
LG