Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:02

Ripoti inayochunguza ufisadi dhidi ya Ramaphosa imetolewa Alhamis


Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa

Matokeo ya jopo hilo yanakuja chini ya mwezi mmoja kutoka kwa mkutano wa uchaguzi ambao utaamua ikiwa Rais Ramaphosa atawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha African National Congress (ANC) katika uchaguzi wa mwaka 2024

Ripoti ya jopo ambalo lilipata ushahidi wa awali kwamba Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa huenda alikiuka kiapo chake cha urais ni "wakati wa kusikitisha" kwa serikali na chama tawala, waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor alisema katika mahojiano yake kwenye mkutano wa Reuters NEXT.

Jopo hilo liliteuliwa na spika wa bunge kuangalia iwapo Ramaphosa anapaswa kukabiliwa na mchakato wa kumuondoa madarakani baada ya mamilioni ya pesa taslimu kudaiwa kuibwa katika shamba lake la kibinafsi mwaka 2020.

Ramaphosa amekana kufanya makosa yoyote na hajashtakiwa kwa uhalifu wowote.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini, Pandor aliongeza kuwa bado anasoma ripoti ya jopo kuhusu wizi huo katika shamba la Ramaphosa na kwamba hakutaka kukimbilia katika anga za umma kwa maoni ya ziada.

Matokeo ya jopo hilo yanakuja chini ya mwezi mmoja kutoka kwa mkutano wa uchaguzi ambao utaamua ikiwa Rais Ramaphosa atawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha African National Congress (ANC) katika uchaguzi wa mwaka 2024.

XS
SM
MD
LG