Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 22:35

Zuma aachiliwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miezi 15 jela


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiingia kwenye mahakama kuu ya mjini Pietermaritzburg, Afrika Kusini, Januari 31, 2022. Picha ya Reuters
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiingia kwenye mahakama kuu ya mjini Pietermaritzburg, Afrika Kusini, Januari 31, 2022. Picha ya Reuters

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameachiliwa huru baada ya muda wake wa kutumikia kifungo jela kumalizika kwa makosa ya kudharau mahakama, wizara ya sheria imesema Ijumaa.

Zuma alihukumia miezi 15 jela mwaka jana baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki kwenye uchunguzi kuhusu ufisadi.

Alijasilimisha mwenyewe Julai 7 kuanza kutumikia kifungo chake, hali ambayo ilichochea ghasia ambazo Afrika Kusini haijawahi kushuhudia katika miaka kadhaa, wakati wafuasi wake wenye hasira walipoingia barabarani kuandamana.

Zuma aliachiliwa huru mwezi Septemba mwaka wa 2021 kutokana na sababu za kiafya. Lakini mwezi Disemba, mahakama ilifutilia mbali msamaha huo na kuamua arejee jela.

Zuma alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo na aliendelea kuwa huru akisubiri maamuzi ya rufaa yake hadi muda umemalizika.

XS
SM
MD
LG