Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:34

Mawakili waeleza wasiwasi juu ya usalama wa mlalamikaji dhidi ya Trump


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Mawakili wanaomwakilisha afisa usalama aliyetoa malalamiko na kupelekea uchunguzi dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump wanaelezea umuhimu wa kulinda jina la mtu huyo.

Rais Trump anasema mlalamikaji huyo ambaye amesababisha kuwepo uchunguzi huo unaotaka kumuondoa madarakani, anahaki ya "kukutana na mtu huyo."

Wakili mwingine, Mark Zaid, alikanusha ripoti kwamba mtoaji siri huyo alikuwa kwenye ulinzi wa serikali kuu kutokana na wasi wasi wa usalama wake.

Kundi la mawakili lilisambaza nakala ya barua walioituma ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa Taifa ikielezea kuongezeka wasi wasi wake juu ya usalama wa mlalamikaji huyo dhidi ya Trump katika kipindi cha wiki iliyopita na wanatarajia hatari hiyo kuongezeka. Walinukuu ushahidi wa tamko la rais. Wanasheria pia walisema wanafahamu kuna watu wanajaribu kutumia fedha nyingi kupata taarifa za jina la mlalamikaji huyo aliyekuwa amepaza sauti.

Timu hiyo ya wanasheria ikiongozwa na Andrew Bakaj ilitoa tamko Jumapili kwamba wanaendelea kufanya kazi na Wademokrat na Warepublikan Bungeni kukamilisha utaratibu wa mtu huyo aliyelalamika kukutana na wawakilishi, lakini tarehe bado haijapangwa.

"Nataka kujua ni nani aliyempa habari hizi mtoa taarifa, ni nani mtu huyu aliyempa mtoa taarifa habari hizi, kwa sababu ni kitendo kinakaribiana na ujasusi. Unajua tulikuwa tunafanya nini zamani wakati tulipokuwa mahiri? Sawa? Majasusi na wahaini, sawa? Tulikuwa tukichua hatua tafauti na kile tunachofanya leo," Trump alisema Alhamisi.

Katika barua nyingine iliyotumwa kwa Wademokrat na Warepublikan wa ngazi ya juu katika kamati za usalama ya Baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi, mawakili wa mlalamikaji huyo wamewataka "kuzungumza juu ya kumlinda mlalamikaji huyo na kusisitiza kuwa huu ni mfumo wa kumhami ambapo hakuna ulipizaji kisasi, iwe wazi au kinyume cha hivyo.

Trump amekuwa akirejea kuandika katika akaunti yake ya Twitter, akitetea mazungumzo yake ya simu ya Julai aliyofanya na Rais wa Ukrain Volodymyr Zelenskiy ambayo ni kiini cha taarifa alizotoa mlalamikaji dhidi ya Trump.

XS
SM
MD
LG