Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:41

Trump kwa UN: Nitasimama imara na sera zangu za "Amerika kwanza"


Rais wa Marekani Donald Trump ahutubia mkutano wa 75 wa Umoja wa Mataifa mjini New York (Sep 24, 2019)
Rais wa Marekani Donald Trump ahutubia mkutano wa 75 wa Umoja wa Mataifa mjini New York (Sep 24, 2019)

Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano alitumia maneno makali dhidi ya serikali ya Iran na kusema kuwa mataifa yote ya ulimwengu yana jukumu la kulaani taifa hilo la Kiislamu.

Akihutubia mkutano wa 75 wa baraza kuu la Umoja wa mataifa nchini New York, Trump, ambaye alitetea sera zake za "kuiweka Marekani kwanza," aidha alisema hakuna serikali yoyote yenye uwajibikaji ambayo inaweza kuunga mkono kile alichokiita ‘kiu ya damu’ iliyo nayo Iran.

Wakati wa hotuba hiyo, rais wa Iran Hassan Rouhani hakuwepo katika ukumbi huo.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, zimeungana na Marekani katika kuishutumu Iran kwa mashambulizi ya hivi karibuni ya vinu vya mafuta vinavyomilikiwa na Saudi Arabia.

Marekani na Iran zimekuwa zikirushiana cheche za maneno kufuatia kuzorota kwa ushirikaiano wa kidiplomasia, hususan baada ya Trump kuiondoa Marekani kwa mkataba wa nyuklia, wa mwaka wa 2015 kati ya Iran na mataifa mengine yenye nguvu za kiuchumi.

Trump alitetea msimamo wake wa kuijali Marekani kwanza kabla ya kuyafikiria mataifa mengine.

"Ukitaka uhuru, jivunie nchi yako. Ukitaka demokrasia, jivunie uhuru wako, na ukitaka amani, ipende nchi yako," alisema.

Hotuba ya Trump, ambayo pia ililenga masuala mengine mbalimbali, pia iligusia uhamiaji, huku akisema sera zinazoungwa mkono na wanaharakati wa mipaka iliyo wazi, zinawaumiza raia na kuwa ni za kishetani.

Amesema sera hizo ni za kuunga mkono magenge ya kihalifu, na kwamba, zinapelekea ukiukaji wa haki za binadamu kwa wale wanaowapokea wahamiaji hao.

Trump pia ameishutumu China na kusema kuwa dunia nzima inatazama kwa karibu kuona jinsi rais Xi Jinping wa nchi hiyo atakavyotatua mzozo unaoikabili Hong Kong.

XS
SM
MD
LG