Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:28

Wademocratic wamemtaka Pompeo kukabidhi nyaraka muhimu bungeni ifikapo Alhamis


Adam Schiff (D) mwenyekiti wa kamati ya ujasusi bungeni. Sept. 19, 2019,
Adam Schiff (D) mwenyekiti wa kamati ya ujasusi bungeni. Sept. 19, 2019,

Wademocratic hao walisema wizara ya mambo ya nje Marekani imekiri kuwa ofisa mwandamizi wa Mike Pompeo alisaidia moja kwa moja kupanga mikutano kati ya mwanasheria wa Rais wa Marekani Donald Trump, Rudy Giuliani na maafisa wa Ukraine

Viongozi watatu wenye nguvu katika bunge la Marekani wanamtaka waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo kuanza kukabidhi nyaraka zote zinazohusiana na mazungumzo ya simu kati ya Trump na Ukraine ifikapo Alhamis au atapatiwa hati ya kuitwa kujieleza.

Wa-Democratic hao ambao wanaongoza kamati ya mambo ya nje, ujasusi na ufuatiliaji ni Elliot Engel, Adam Schiff na Elijah Cummings walisema kwanza waliwasilisha ombi lao kwa njia ya barua kwenda wizara ya mambo ya nje Marekani wiki mbili zilizopita.

Elijah Cummings (D) mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji bungeni
Elijah Cummings (D) mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji bungeni

Walisema wizara hiyo imekiri kwamba ofisa mwandamizi wa Pompeo alisaidia moja kwa moja kupanga mikutano kati ya mwanasheria wa Rais wa Marekani Donald Trump, Rudy Giuliani na maafisa wa Ukraine siku kadhaa baada ya Rais Trump kuzungumza kwa njia ya simu na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy.

Viongozi hao watatu walisema kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Giuliani, binafsi aliwaeleza maafisa wawili wa vyeo vya juu wa wizara ya mambo ya nje Marekani kuhusu mkutano wake.

Rais Trump anakiri yeye na Zelenskiy walizungumza kuhusu rushwa na pia suala la mgombea urais wa Democratic, Joe Biden wakati wa mazungumzo yao kwa njia ya simu ya Julai 25.

XS
SM
MD
LG