Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:13

Marekani yaweka msimamo wake wazi juu ya Taiwan


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden, amesema kwamba yupo tayari kuilinda Taiwan kwa nguvu.

Hatua hiyo imepokelewa vyema na utawala wa kisiwa cha Taiwan huku ikikosolewa vikali na China.

Katika kikao na waandishi wa habari, akiwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, Biden amesema kwamba Marekani itakuwa tayari kuilinda Taiwan iwapo itashambuliwa.

Rais Biden alieleza haya: "Tunaunga mkono sera ya China moja, tunaunga mkono yote ambayo tumefanya katika miaka iliyopita, lakini hilo halina maana kwamba China ina haki ya kutumia nguvu na kuiteka Taiwan. Kwa hivyo tunaunga mkono Japan na mataifa mengine kuhakikisha kwamba hilo halifanyiki.

Ramani ya Taiwan
Ramani ya Taiwan

Na matarajio yangu kwamba hili halitatokea, wala lisijaribiwe. Matarajio yangu kuwa kuna mengi ambayo yanategemea namna dunia itachukua msimamo dhidi ya hatua kama hiyo n akutambua kwamba inaweza kusababisha madhara ya muda mrefu katika jamii.

Akiwa kwenye ziara yake ya kwanza nchini Japan tangu alipoingia madarakani, Biden amesema kwamba hana matarajio kwamba kitu kama hicho kinaweza kutokea au mtu kufikiria kukifanya.

Wizara ya mambo ya nje ya Taiwan imemshukuru Biden kwa kuhakikisha msaada wake kwa kisiwa hicho endapo kitavamiwa na Beijing.

Hata hivyo, wizara ya mambo ya nje ya China imeeleza kutofurahishwa na matamshi ya Biden, ikisema kwamba Beijing haina nafasi ya kulegeza msimamo wake kuhusiana na maswala ya uhuru wa mipaka.



XS
SM
MD
LG