“Leo, Rais Yoon na mimi tumejitolea kuimarisha ushirikiano wetu wa karibu na kufanya kazi pamoja ili kukabiliana na changamoto za usalama wa kikanda, ikiwa ni pamoja na kushughulikia tishio la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea kwa kuimarisha zaidi namna yetu ya kujihami na kufanya kazi kuelekea kuondoa kabisa nyuklia katika Peninsula ya Korea” alisema Biden Jumamosi katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Seoul, katika hatua ya kwanza ya ziara yake ya siku sita huko Korea Kusini na Japan.
Rais Biden alithibitisha kujitolea kwa Marekani kwa utetezi wa Jamhuri ya Korea na kujihami kwa muda mrefu," Yoon alisema kupitia mkalimani. Kujihami kwa muda mrefu ni neno linaloonyesha Marekani itatumia uwezo wake kamili wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa nyuklia, wa kawaida na wa makombora katika kutetea washirika wake.