Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:58

Waziri mkuu mpya wa Australia kukutana na Biden, Japan


Waziri mkuu mpya wa Australia Anthony Albanese
Waziri mkuu mpya wa Australia Anthony Albanese

Waziri mkuu mpya wa Australia Anthony Albanese ameapishwa mapema Jumatau kabla ya kuelekea Japan kwa mazungumzo na rais wa Marekani Joe Biden pamoja na viongozi wengine wa dunia.

Kiongozi huyo wa chama cha Labor aliibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa Jumamosi na hivyo kufikisha kikomo utawala wa karibu muongo mmoja wa kikonsavative. Serikali ya Albanese ya mrengo wa kushoto kati sasa inakabiliwa na changmoto za sera za mambo ya nje ikiwemo kuimarisha uhusiano na China.

Kiongozi huyo amsema kwamba kuimarisha ushirikiano na Beijing ni kibarua kigumu ikizingatiwa tofauti za kieneo na kisiasa, zilizoshuhudiwa katika miaka ya karibuni. Wachambuzi wa siasa wanasema kwamba wanatarajia serikali ya Albanese kulenga kuimarisha diplomasia na mataifa ya kusini na mashariki mwa Asia, ili kudhibiti ushawishi wa China.

Albanese anatarajiwa kuhudhuria kikao cha mataifa manne Jumanne mjini Tokyo atakapokuwa Joe Biden pamoja na viongozi wa India na Japan.

XS
SM
MD
LG