Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:31

Marekani yafungua mkutano wake wa pili juu ya Demokrasia duniani


Presidenti Biden
Presidenti Biden

Marekani Jumanne inafungua mkutano wake wa pili juu ya Demokrasia ikiangazia kwa makini nchi nyingine duniani, ikijenga msimamo wa pamoja dhidi ya udikteta wa Russia katika uvamizi wake nchini Ukraine na wakati China ikianza hujuma yake ya kidiplomasia.

Rais Joe Biden alichukua madaraka kwa ahadi ya kuhamasisha demokrasia, na katika mwaka wake wa kwanza amepiga hatua nzuri kwa uzinduzi wa mkutano huu, unaotaka kuthibitisha tena uongozi wa Marekani duniani.

Katika kipindi hiki, ikiitikia wasiwasi ulioelezwa kuwa mkutano wa kwanza ulikuwa umejikita zaidi juu ya Marekani, Biden amechagua waendeshaji wenza wa mkutano huu kutoka kila bara – marais wa Zambia, Costa Rica na Korea Kusini na waziri mkuu wa Uholanzi.

Kwa ujumla, amewaalika viongozi 121 kwa siku hizo tatu za mkutano, wengi wao kwa njia ya mtandao – viongozi wanane zaidi kuliko wale wa 2021.

Mkutano wa kilele unakuja wakati tishio kwa demokrasia linafukuta “katika kile kilichoonekana kama ni suala muhimu, ikiwa ni tishio linalosogea taratibu, kuelekea lile ambalo hivi sasa ni muhimu na la dharura sana,” alisema Marti Flacks, mkurugenzi wa juhudi za kuimarisha haki za binadamu katika kituo cha utafiti wa masuala ya kimkakati na kimataifa.

Vikao hivyo vitawaleta wawakilishi wa jumuiya za kiraia kwa majadiliano kuhusu changamoto mbalimbali hadi masuala ya demokrasia ikiwemo teknolojia ya kukusanya taarifa, ambayo Marekani inaiona ni tishio linaloongezeka wakati China ikipiga hatua mbalimbali katika teknolojia kama hizo.

“Kutokana na kutokuwepo hatua ya bunge katika nyanja hiyo, ni muhimu kuwa utawala huu unafanya mawasiliano ya pande mbili na nchi nyingine na pia makampuni kuchukua hatua za kujitolea ambazo zinaweza kuchukuliwa katika kipindi cha mpito,” Flacks alisema.

Mkutano huo utafunguliwa Jumanne kwa mazungumzo kwa njia ya mtandao juu ya amani nchini Ukraine ikimshirikisha Rais Volodymyr Zelenskyy

Siyo tu ujumbe huo lakini mpangilio utakuwa na muonekano tofauti ukilinganisha na mkutano ule wa kwanza ambapo Zelenskyy, hivi sasa ni kiongozi wa kipindi cha vita akiwa katika mavazi ya kijeshi, alikuwa amenyowa ndevu, na kuvaa suti nyeusi iliyonyooshwa vizuri.

Wakati Biden akiwa ameendeleza ahadi zake za kampeni juu ya mkutano wa demokrasia, amewasikitisha baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu kwa kulegeza msimamo wa ahadi yake ya awali kuwaepuka viongozi madikteta.

Mwaka 2022 Biden aliitembelea Saudi Arabia, na kutambua mchango wa ufalme huo katika masoko ya mafuta, na kwenda Misri, mwenyeji wa mkutano wa hali ya hewa na mshirika wa Marekani katika usalama wa kieneo, na ameongeza kushirikiana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan juu ya suala la Ukraine.

Nchi zote hizi tatu hazijaalikwa katika mkutano huo, ukosoaji hasa wa Erdogan, ambaye anagombea tena katika uchaguzi wa Mei 14 baada ya miongo miwili akiwa madarakani na akishutumiwa kuendeleza udikteta.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG