Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:24

Rais wa Israeli aeleza ubadilishaji mfumo wa mahakama ni 'makosa'


Rais wa Israeli Isaac Herzog
Rais wa Israeli Isaac Herzog

Msukumo huo wa serikali yenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kutaka kufanya mabadiliko katika mahakama za Israeli imesababisha hasira ndani ya nchi na wasiwasi miongoni mwa nchi za Magharibi ambazo ni washirika wake.

Iwapo pendekezo hilo litapita, itamaanisha serikali kwa kiwango kikubwa itakuwa na nguvu ya kuchagua majaji na kuminya nguvu za Mahakama ya Juu kufuta sheria.

Baada ya wiki kadhaa za maandamano nchi nzima ambayo yamedhihirisha mgawanyiko mkubwa katika jamii ya waisraeli, Rais Isaac Herzog, ambaye amekuwa mpatanishi kati ya pande hizo mbili, alionya katika hotuba kwa njia ya televisheni kwa taifa kutokea balaa.

Alisema Israeli imefikia “hatua ya kutorudi nyuma” na kutaka serikali ya mseto kufikiria tena pendekezo la sheria hiyo, ambapo linaungwa mkono vikali na vyama vinavyo simamia utaifa na udini.

“Ni makosa, ni hatua kali, inadumaza misingi yetu ya kidemokrasia. Kwa hiyo ni lazima kuwe na kitu mbadala, kinachokubalika kiwekwe wazi mara moja,” Herzog alisema.

Wakati Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliondoka kuelekea katika ziara ya Rome, ilibidi awakwepe Waisraeli waliokuwa wanapeperesha bendera ambao walifurika katika njia zote zinazoelekea uwanja wa ndege wa Ben Gurion akiwa katika msafara wa magari.

Kabla ya kuondoka, alifanikiwa kusalimiana na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ambaye alielezea wasiwasi wa Washington kuhusu pendekezo hilo dhidi ya mahakama akisema kuwa pande zote za demokrasia ya Marekani na Israel zilikuwa zimejengwa kwa misingi ya mahakama huru.

Chanzo cha habari hii inatokana na shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG