Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:14

Israel na Sudan zafikia makubaliano kurejesha uhusiano wa kawaida


Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Taifa Eli Cohen (left) akibadilishana nyaraka na Waziri wa Ulinzi wa Sudan Ibrahim Yasin wakati walipokutana mjini Khartoum, Sudan January 25, 2021.
Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Taifa Eli Cohen (left) akibadilishana nyaraka na Waziri wa Ulinzi wa Sudan Ibrahim Yasin wakati walipokutana mjini Khartoum, Sudan January 25, 2021.

Israel na Sudan zilikubaliana kuendelea na juhudi za kurejesha uhusiano wa kawaida  kati yao wakati wa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Israel Eli Cohen mjini Khartoum siku ya Alhamisi, wizara ya mambo ya nje ya Sudan ilisema.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa afisa wa Israel kutambuliwa rasmi na Sudan, ingawa kumekuwa na mfululizo wa mazungumzo kati ya maofisa wa nchi hizo mbili katika miaka ya karibuni.

Sudan ilikubali kuchukua hatua za kurejesha uhusiano wa kawaida na Israel katika makubaliano ya mwaka 2020 yaliyosimamiwa na utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, sambamba na mikataba ya kurejesha uhusiano kati ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Morocco, iliyojulikana kama “Abraham Accords”.

Mwezi Januari 2021, Sudan ilisema aliyekuwa waziri wake wa sheria Nasredeen Abdulbari, wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin nchini, alisaini mkataba wa Abraham Accords.

Cohen na mkuu wa baraza la utawala la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan walijadili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika masuala ya usalama na kijeshi, na pia katika kilimo, nishati, afya, maji na elimu. Taarifa ya ofisi ya Burhan ilisema.

Hakuna majibu ya mara moja kutoka kwa maafisa wa Israeli, lakini Ofisi ya Cohen ilisema kuwa ataitisha mkutano na waandishi wa habari jioni " atakaporejea kutoka katika ziara ya kihistoria ya serikali". Lakini hakufafanua.

Cohen alifanya ziara ya kwanza nchini Sudan mwaka 2021 wakati alipokuwa waziri wa ujasusi.

Jeshi la Sudan ambalo limekuwa likitawala nchi hiyo tangu mapinduzi ya Oktoba 2021, linasema linakusudia kukabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia, na inaonekana kuongoza hatua hiyo kuelekea kuanzisha mahusiano na Israeli.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG