Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:48

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken awasili Mashariki ya Kati


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken akishiriki katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria matukio katika Mkutano wa 55 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa ASEAN mjini Phnom Penh mnamo Agosti 5, 2022. (Picha na Tang Chhin Sothy / AFP).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken akishiriki katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria matukio katika Mkutano wa 55 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa ASEAN mjini Phnom Penh mnamo Agosti 5, 2022. (Picha na Tang Chhin Sothy / AFP).

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken aliwasili Mashariki ya Kati leo Jumapili, akianza ziara ya siku tatu huku ghasia zikipamba moto kati ya Waisraeli na Wapalestina, na huku Iran na vita vya Ukraine vikiwa katika ajenda ya juu.

Baada ya kusimama mjini Cairo Blinken ataelekea Jerusalem siku ya Jumatatu, ambako serikali mpya ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya mrengo wa kulia imezua wasiwasi ndani na nje ya nchi hiyo kuhusu mustakabali wa maadili yasiyo ya kidini ya Israel, kuvuruga uhusiano wa kikabila na kukwamisha mazungumzo ya amani na Wapalestina.

Pia kumekuwa na msururu wa ghasia mbaya katika siku za hivi karibuni, na hivyo kuzidisha hofu kwamba ghasia ambazo tayari zimeshamiri zitaongezeka zaidi.

Mtu aliyekuwa na silaha raia wa Palestina aliwaua watu saba katika shambulizi nje ya sinagogi la Jerusalem siku ya Ijumaa. Lilikuwa shambulio baya zaidi kama hilo dhidi ya Waisraeli katika eneo la Jerusalem tangu mwaka 2008 na lilifuatia shambulio baya la Israel katika mji unaokaliwa kimabavu wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin siku ya Alhamisi, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka kadhaa.

XS
SM
MD
LG