Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:20

Iran yakasirishwa na maoni ya Ukraine 


Iran imemuita mkuu wa ubalozi wa Ukraine mjini Tehran Jumatatu kuhusiana na maoni ya nchi yake juu ya shambulio la ndege isiyo kuwa na rubani katika kiwanda cha kijeshi kwenye jimbo la katikati la Isfahan, kulingana na Shirika la habari la Tasnim.

Ukraine, ambayo inaishutumu Iran kupeleka mamia ya ndege zisizo na rubani kwa Russia ili kushambulia malengo ya kiraia katika miji ya Ukraine iliyo mbali na mstari wa mbele wa vita, msaidizi wa ngazi ya juu wa Rais Volodymyr Zelenskyy amelihusisha tukio hilo moja kwa moja na vita vya huko.

“Usiku wa mlipuko nchini Iran,” Mykhailo Podolyak alitweet Jumapili. "Nilikuonya."

Afisa mmoja wa Marekani ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba Israel inaonekana kuhusika na shambulio hilo.

Iran imekiri kutumia ndege zisizo na rubani kwenda Russia lakini imesema ndege hizo zilitumwa kabla ya Moscow haijafanya uvamizi wake Ukraine mwaka jana.

Moscow imekanusha majeshi yake kutumia ndege zisizo na rubani kutoka Iran kuishambulia Ukraine. Hata hivyo ndege nyingi zimetunguliwa na kuchukuliwa.

XS
SM
MD
LG