Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:27

Wananchi wakusanyika nje ya bunge la Israeli kupinga kuapishwa kwa baraza jipya


Bunge la Israeli.
Bunge la Israeli.

Maelfu ya waisraeli wameandamana nje ya bunge la Israel, wakati baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu linaapishwa, kupinga kuapishwa kwa baraza hilo jipya.

Maelfu ya watu wameandamana nje ya bunge la Israel, wakati baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu linaapishwa, kupinga kuapishwa kwa baraza hilo.

Netanyahu anatarajiwa kurudi madarakani akiapa kutekeleza sera ambazo zinaweza kusababisha migogoro ndani na nje ya Israel, na kupelekea Israel kutengwa na washirika wake wa karibu.

Viongozi wa upinzani wa Israel wameelezea kupinga kabisa msimamo wa Netanyahu wakati anatarajia kutangaza sera zake kwa taifa.

Serikali mpya imeapishwa hii leo. Waandamanaji waliopeperusha bendera wamepaaza sauti wakiushutumu utawala wa Netanyahu kwa ubaguzi. Mmoja wa waandamanaji Dania Meirovich asema:

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

"Serikali mpya ambayo inatarajiwa kuapishwa inajaribu kupitisha sheria zenye ubaguzi dhidi ya watu walio katika uhusiano ya mapenzi ya jinsia moja, waarabu, wanawake na mtu yeyote ambaye ni tofauti.

Serikali mpya ya Netanyahu imeahidi kwamba itazingatia zaidi upanuzi wa makaazi ya watu huko Ukingo wa Magharibi, kuweka ruzuku kwa washirika wake wa Orthodox na kuleta mabadiliko makubwa katika idara ya mahakama.

Wanaopinga mipango hiyo wanasema kwamba hatua hizo zinasababisha taasisi za demokrasia kukosa nguvu.

Netanyahu ni waziri mkuu wa Israel ambaye ametawala nchi hiyo kwa muda mrefu. Alikuwa madarakani miaka ya 1990 na kabla ya kurejea kati ya mwaka 2009 na 2021.

XS
SM
MD
LG