Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:53

Marekani: Kufufuliwa tena kwa makubaliano ya nyuklia na Iran 'siyo lengo letu...'


Ned Price
Ned Price

Marekani Jumatano ilisema kufufuliwa tena kwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ya 2015 “siyo lengo letu hivi sasa,” ikisema kwamba Tehran ilikuwa imeonyesha utashi mdogo katika kufufua mkataba huo na kuwa “Washington imejikita katika kuangalia jinsi ya kuwasaidia waandamanaji nchini Iran.

Akiulizwa iwapo Marekani ina utashi wa kuendelea na mazungumzo ili kufufua mkataba huo ambao Iran ilisitisha programu yake ya nyuklia kwa kupatiwa afueni ya vikwazo vya uchumi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alijibu, “hilo silo tunaloshughulika nalo hivi sasa.

“Ni wazi kuwa, na pia Wairan wameweka wazi kuwa haya siyo makubaliano ambayo wako tayari kuyafanya. Bila shaka makubaliano haya hayaonyeshi kutokea mara moja,” Price alieleza mkutano.

“Hakuna tulichosikia wiki za karibuni kinachoeleza kuwa wamebadilisha msimamo wao. Na hivyo hivi sasa, tunajikita… katika ushujaa dhahiri na ushupavu wananchi wa Iran wanaonyesha kupitia maandamano yao ya amani,” alisema.

Maandamano yanayoendelea nchini Iran.
Maandamano yanayoendelea nchini Iran.

“Tunajikita hivi sasa kuangazia yale wanayofanya na kuwasaidia katika njia tunazoweza,” alisema, akikusudia maandamano ya kuipinga serikali yaliyoibuka kufuatia kifo cha Mahsa Amini, 22, akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili.

Rais wa zamani Marekani Donald Trump aliachana na makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani mwaka 2018 na yeye peke yake aliwawekea vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimezorotesha uchumi wa Iran kwa kuzuia usafirishaji wao wa mafuta nje.

Mwaka moja baadae, Tehran ilikaidi kwa kuanza kukiuka makubaliano ya kiwango cha nyuklia, hofu ya Marekani, Israeli na nchi za Ghuba ya Kiarabu kuwa Iran inaweza kuwa inaelekea kumiliki silaha za atomiki, matakwa ambayo Iran inayakanusha.

XS
SM
MD
LG