Iran imeanzisha kampeni mpya ya mashambulio ya mabomu kwa kutumia ndege zisizo na rubani Jumatano ikilenga maeneo ya makundi ya upinzani ya Kikurdi.
Maeneo hayo yapo kaskazini mwa Iraq wakati ambapo kuna maandamao ya kuipinga serekali ya kislamu wamesema maafisa wa Kikurdi.
Mashambulizi yamefanyika mapema Jumatano yakilenga Koya iliyopo kilometa 60 mashariki mwa Irbil amesema Soran Nuri, mwanachama wa chama cha Demokratik cha Kikurdi cha Iran.
Kundi hilo linalo fahamika kama KDPI ni kundi la mrengo wa kushoto lenye silaha ambalo limepigwa marufuku Iran.
Shirika la habari linalo endeshwa na serekali la IRNA na mashirika ya utangazaji yamesema kwamba vikosi vya nchi kavu vya serekali ya kimapinduzi vililenga baadhi ya kambi ya makundi ya uasi kaskazini mwa Iraq kwa kutumia makombora yenye usahihi na ndege zisizo na rubani za kushambulia.