Wakati maandamano yakiendelea katika miji na majiji ya Iran kwa wiki ya nne, maelefu ya Wairan wanaoishi nje ya nchi wameandamana katika mitaa ya Ulaya, Amerika Kaskazini na kwingineko.
Maandamano hayo ni kuunga mkono kile wengi wanaamini kuwa ni wakati wa kusafisha taifa lao.
Kuanzia wale walio kimbia miaka ya 1980 baada ya mapinduzi ya Kislamu ya mwaka 1979 mpaka vizazi vipya vya Wairan waliozaliwa nje ya nchi na kukulia katika mataifa ya magharibi wanasema wameona mshikamano ambao haujawahi kutokea.
Wanasema mshikamano huo unaendana na nia dhabiti katika kupinga kifo cha binti wa miaka 22 ambaye alikuwa akishikiliwa na polisi wa usimamizi wa mila na desturi.
Katika miezi ya karibuni mikusanyiko mikubwa ya raia wenye asili ya Iran katika dazeni ya miji kuanzia London, Paris mpaka Toronto imeshuhudiwa ikitoa mshikamano wa kupinga kilichotokea na kusababisha kifo cha Mahsa Amini akiwa mikononi mwa polisi