Kampuni iliyoorodheshwa na London ya Energean siku ya Jumapili ilianza kufanya majaribio ya mabomba kati ya Israel na kinu cha gesi cha pwani ya Karish ikiwa hatua muhimu kuelekea uzalishaji kutoka eneo la mashariki mwa Mediterranean moja ya chanzo cha mivutano kati ya majirani Israel na Lebanon.
Israel imeshikilia kuwa Karish iko kabisa ndani ya eneo lake na sio suala la mashauriano yanayoendelea ambayo yanasimamiwa na marekani juu ya mpaka wa baharini na Lebanon. Nchi hizo mbili kiufundi bado ziko vitani.
Lebanon imeripotiwa kudai baadhi ya maeneo ya Karish na kundi la Kishia la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran ambalo lina ushawishi mkubwa nchini Lebanon hapo awali lilitishia mashambulizi iwapo Israel itaanza uzalishaji kwenye eneo hilo.
Katika taarifa ya Jumapili, Energean ilisema kuwa "kufuatia idhini iliyopokelewa kutoka Wizara ya Nishati ya Israeli kuanza taratibu kadhaa za majaribio, mtiririko wa gesi kutoka pwani hadi FPSO umeanza", akimaanisha kituo cha kuhifadhi uzalishaji cha Karish.