Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:46

Wanamgambo watatu wauwawa Palestina na vikosi vya Israel


Vikosi vya Israel, vilivamia kijiji cha Wapalestina karibu na mji wa Ukingo wa Magharibi, Jenin, Alhamisi na kuwaua wanamgambo watatu wa kijihadi ambao walishukiwa kufanya mashambulizi ya risasi katika eneo hilo.

Kundi la Islamic Jihad limewatambua wapiganaji hao watatu, ambao jeshi la Israel, lilisema wanashukiwa kufanya mashambulizi mengi ya risasi katika kijiji cha Jaba, kusini magharibi mwa Jenin, na pia katika eneo la Homesh, kituo cha makazi cha karibu ambacho kilihamishwa 2005 na sasa ni sehemu ya shule ya kidini.

Tukio limetokea siku moja na ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, Israel, ambapo alitarajiwa kuzungumzia ghasia zinazo ongezeka kwenye Ukingo wa Magharibi.

Huko Jaba, wakaazi wamesema walisikia milio ya risasi asubuhi na mapema na kuona jeshi la Israeli katika kijiji hicho, ambapo mabaki ya gari la watu wenye silaha waliuawa yalibaki barabarani.

XS
SM
MD
LG