Leaf ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba baada ya juhudi za miaka kadhaa kujenga demokrasia ya Tunisia, kuna hatua zinazoonekana ambazo zimechukuliwa na Kais katika muda wa mwaka mmoja na nusu uliopita, ambazo zinaipeleka nchi hiyo katika njia isiyo sahihi.
Saied aliingia madarakani mwaka 2021, na kulivunja bunge kabla ya kuidhinisha katiba mpya ambayo inampa madaraka makubwa.
Wanasiasa kadhaa wa upinzani wamekamatwa mwaka huu, wakishutumiwa kwa njama za kupanga mapinduzi.
Saied amesema kwamba anafanya maamuzi yake kulingana na sheria ni muhimu kutuliza hali ya siasa nchini Tunisia baada ya migogoro ya muda mrefu.
Amewashutumu wapinzani wake akiwataja kuwa wahalifu, wasaliti na magaidi. Ametangaza msako dhidi ya wahamiaji akisema kwamba ni wahalifu.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.