Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:38

Tunisia: Waandamanaji wakaidi amri licha ya viongozi wao kukamatwa


Waandamanaji nchini Tunisia.
Waandamanaji nchini Tunisia.

Mamia ya wafuasi wa upinzani nchini Tunisia walikaidi marufuku rasmi ya maandamano dhidi ya rais siku ya Jumapili baada ya baadhi ya viongozi wao kukamatwa, na kuvunja kizuizi cha polisi katikati mwa Tunis wakiandamana katika barabara kuu ya mji huo.

Mamia ya wafuasi wa upinzani nchini Tunisia walikaidi marufuku rasmi ya maandamano dhidi ya rais siku ya Jumapili baada ya baadhi ya viongozi wao kukamatwa, na kuvunja kizuizi cha polisi katikati mwa Tunis wakiandamana katika barabara kuu ya mji huo.

Kabla ya waandamanaji hao kuvunja kizuizi hicho, polisi waliwaonya kwa vipaza sauti kwamba maandamano yao ni kinyume cha sheria lakini wakaongeza kuwa hawatawazuia kwa nguvu.

Takriban waandamanaji elfu moja walijazana kwenye Barabara ya Habib Bourguiba ambapo mikutano mingi hufanyika, wakiimba "Zima mapinduzi" na "Tunataka kuachiliwa kwa waliokamatwa."

Muungano wa National Salvation Front unajumuisha chama kikubwa zaidi cha Tunisia, Islamist Ennahda, vuguvugu la waandamanaji la Stop the Coup na baadhi ya vyama vingine vya kisiasa, vinavyomtaka Rais Kais Saied ajiuzulu.

Ingawa yalikuwa kati ya maandamano madogo kabisa ya muungano huo dhidi ya Saied, bado muungano huo ulionyesha una uwezo wa kuwaleta pamoja waandamanaji kudai matakwa yao, huku polisi wakionyesha kuwa bado hawakuwa tayari kusitisha maandamano kwa nguvu.

"Tuko hapa tena licha ya kampeni inayolenga kuwakamata wapinzani. Tutaendelea kupinga hatua kuwaachilia wafungwa walio kizuiziani, lakini pia kukabiliana na mapinduzi," alisema Nejib Chebbi, kiongozi wa National Salvation Front ambaye kaka yake amekamatwa.

Katika wiki za hivi karibuni, baadhi ya viongozi wakuu wa kundi hilo wamezuiliwa kama sehemu ya msako mkali dhidi ya wakosoaji mashuhuri wa Saied, na kushtakiwa kwa kula njama dhidi ya usalama wa serikali. Wiki hii, gavana wa Tunis alikataa kutoa kibali cha maandamano ya Jumapili.

XS
SM
MD
LG