Takriban watu 50 wakiwemo watoto 11 walikuwa wamejikunyata mbele ya ubalozi wa Ivory Coast mjini Tunis, mwandishi wa AFP alisema.
Wakiwa wamejifunika na mablanketi kwa sababu ya upepo wa baridi, watu hao walisema walikuwa wamelala nje kwa siku nne.
Tunahitaji nepi na maziwa ya watoto, hatuna chakula, alisema Rokhia Kone, mwenye umri wa miaka 23, raia wa Ivory Coas akiwa na mtoto wake mgongoni.
Wanaume kadhaa walionyesha vipande vya mkate vilivyopelea ambavyo walisema vingekuwa chakula chao cha pekee kwa siku hiyo.