Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:25

Rais wa Tunisia atuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi


Rais wa Tunisia Kais Saied akipiga kura katika kituo cha kupigia kura, wakati wa kura ya maoni kuhusu katiba mpya, mjini Tunis, Tunisia Julai 25, 2022. Urais wa Tunisia. REUTERS
Rais wa Tunisia Kais Saied akipiga kura katika kituo cha kupigia kura, wakati wa kura ya maoni kuhusu katiba mpya, mjini Tunis, Tunisia Julai 25, 2022. Urais wa Tunisia. REUTERS

Kundi maarufu la kutetea haki za binadamu lilimtuhumu Rais Kais Saied wa Tunisia kwa ubaguzi wa rangi na matamshi ya chuki siku ya Jumatano baada ya kuapa kuwachukulia hatua kali wahamiaji wa Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Saied, ambaye amechukua karibu mamlaka yote tangu hatua ya Julai 2021 dhidi ya bunge, alikuwa amelitaka baraza lake la usalama la kitaifa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na wimbi la wahamiaji.

Makundi ya wahamiaji haramu kutoka Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa bado yanawasili, pamoja na ghasia zote, uhalifu na mazoea yasiyokubalika ambayo yanahusisha, alisema, kulingana na taaŕifa kutoka ofisi yake Jumanne jioni.

Njama ya uhalifu imekuwa ikiendelea tangu mwanzoni mwa karne kubadilisha muundo wa idadi ya watu wa Tunisia aliongeza.

Kauli hiyo ilizua kilio mtandaoni, ambapo wengi walimshutumu rais huyo kwa ubaguzi wa rangi na kuibua nadharia za njama za mrengo wa kulia.

XS
SM
MD
LG