Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:17

Marekani yaipongeza Nigeria kwa uchaguzi mkuu na kutoa wito wa utulivu


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza na waandishi wa habari White house mjini Washington Dc. March 1, 2023. AP
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza na waandishi wa habari White house mjini Washington Dc. March 1, 2023. AP

Marekani siku ya Jumatano iliipongeza Nigeria kwa kuchaguliwa kwa mgombea urais wa chama tawala Bola Tinubu, huku ikitoa wito wa utulivu huku kukiwa na shutuma za wizi wa kura na wasiwasi juu ya hitilafu za kiufundi.

Tinubu alitangazwa mshindi Jumanne kutokana na uchaguzi wa Februari 25 katika nchi ya kidemokrasia yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Marekani inawapongeza watu wa Nigeria rais mteule Tinubu na viongozi wote wa kisiasa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price alisema.

Uchaguzi huu wenye ushindani unawakilisha kipindi kipya cha siasa za Nigeria na demokrasia aliongeza.

XS
SM
MD
LG