Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:53

Waalimu wagoma Sudan wakidai mishahara


Mwanamume akipeperusha bendera ya taifa karibu na matairi yanayowaka wakati wa maandamano katika mji Khartoum kupinga mapinduzi ya kijeshi, Machi 24, 2022. Picha na AFP.
Mwanamume akipeperusha bendera ya taifa karibu na matairi yanayowaka wakati wa maandamano katika mji Khartoum kupinga mapinduzi ya kijeshi, Machi 24, 2022. Picha na AFP.

Waalimu katika shule za serikali nchini Sudan wamekuwa kwenye mgomo tangu Novemba kutokana na mishahara midogo na kutolipwa ujira wao. Wanaishutumu serikali ya kijeshi kwa kushindwa kuweka kipaumbele kwenye elimu na wanataka kurejeshwa kwa serikali ya kiraia.

Wakati huo huo, waziri wa fedha wa Sudan anasema serikali imekidhi madai ya waalimu.

Shule hazina wanafunzi ambao ni kawaida kuonekana kote nchini Sudan. Tangu Novemba, waalimu wameitisha migomo kadhaa, wakipinga mishahara kwamba katika baadhi ya kesi hawalipwi kwa miezi kadhaa, na waalimu wanasema ni midogo mno.

Khamis Maamour Chatmi ni mkuu wa hii shule mjini Khartoum. Anasema ana wasi wasi kuhusu elimu ya wanafunzi wakati mgomo unaendelea. “Tatizo litaharibu vizazi kadhaa na jamii kwa jumla. Tatizo siyo tu linawahusu waalimu wa Sudan lakini jamii nzima,” ameongezea Chatmi.

Wanafunzi wake kama Amir Mohammed Abdalla, wana wasi wasi kuhusu elimu yao pia na shule binafsi zinaendelea na masomo yao na bado zinafundisha, wakati shule za umma, masomo yamesitishwa. Hii kwa kweli ni mbaya sana kwa vile tunataka kuwepo na fursa sawa za kimasomo. Itakuwa ni ushindani na kusababisha mwanya kati yetu,” aliongezea.

Tangu serikali ya kijeshi inayoongozwa na Abdel Fattah al-Burhan alipochukua madaraka kwa njia ya mapinduzi Oktoba mwaka 2021, maandamano ya kuunga mkono demokrasia yameigubika Khartoum takriban kila siku.

Wafanyakazi wa serikali pia wamekumbwa na kutolipwa mishahara yao.

Wenyeji wa Khartoum na hata baadhi ya maafisa wa serikali wameiambia VOA kuna dhana kwamba serikali haifanyi kazi. Mgomo wa waalimu huenda ukawa ni moja ya mambo makubwa.

Gamaria Omar Ahmad Hussain ni makamu mwenyekiti wa Kamati wa Waalimu Sudan, ambayo iliandaa migomo. Anasema hali huenda inaweza kusuluhishwa chini ya serikali ya kiraia.

Hussain anasema “kwasababu tulikuwa na serikali ya kiraia ambayo ilijali kuhusu elimu, kinyume na serikali iliyowekwa baada ya mapinduzi. Ni Dhahiri baada ya mapinduzi, elimu na nyanja nyingine zimeathiriwa…elimu siyo kipaumbele chao hata kidogo kulinga na kile Jibril alichosema katika hotuba yake. Anadhani kwamba elimu na waalimu hawana tija.”

Jibril Ibrahim ni waziri wa fedha wa Sudan, ambaye amekuwa akifanya mashauriano na waalimu kwa niaba ya serikali. Akiongea na VOA, alisisitiza kwamba serikali ilishughulikia matatizo ya waalimu, ambayo anadai wanadanganya.

“Kwa kweli tumeongeza bajeti kwa elimu kwa kiasi cha asilimia 18 hivi sasa. Kwa kiasi jambo zima la madai ya waalimu yanahusishwa na siasa. Kwa kweli, madai yao yameshughulikiwa, lakini baadhi wanatumia madai haya kwa ajenda zao za kisiasa,” amesema Waziri wa Fedha.

Bado migomo inaendelea. Ingawaje mishahara inaonekana kuwa imelipwa kwa waalimu mjini Khartoum, hawajalipwa bado katika sehemu nyingine za nchi, kwa mujibu wa waalimu.

XS
SM
MD
LG