Serikali ya taifa jipya lililoundwa Afrika la Sudan Kusini, itafuta mpango wa mafunzo kwa lugha ya kiarabu katika shule zake, na kuweka ki-Ingereza.
Chini ya mswaada uliopitishwa bungeni wiki hii, masomo yote yatafundishwa kwa lugha ya ki-ingereza. Kiarabu kitakuwepo kama somo, pamoja na masomo ya kawaida kama hesabu na sayansi.
Serikali ya Sudan Kusini inasema mfumo wa lugha ya kiarabu ulilazimishwa mashuleni wakati nchi ilipokuwa sehemu ya Sudan. Sudan Kusini ilijitangazia uhuru kutoka kwa waislam walio wengi nchini Sudan mwezi Julai.
Kura ya maoni ya uhuru ilikuwa sehemu ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini. Lakini mivutano bado ipo kati ya maeneo hayo mawili juu ya masuala ambayo hayajapatiwa ufumbuzi ya namna ya kushirikiana mapato ya mafuta.
Serikali ya Sudan Kusini itaanza kufundisha lugha ya ki-ingereza kwa mashule yote nchini humo