Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:55

Marekani: Jaji Thomas yaelezwa hakuripoti safari kadhaa za kifahari alizofadhiliwa


FILE - Justice Clarence Thomas sits during a group photo at the Supreme Court in Washington, April 23, 2021.
FILE - Justice Clarence Thomas sits during a group photo at the Supreme Court in Washington, April 23, 2021.

Jaji wa Mahakama ya Juu Clarence Thomas kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili kila mwaka amekuwa akikubali ufadhili wa  safari za kifahari kutoka kwa mchangiaji mkuu wa Chama cha Republikan Harlan Crow bila ya kuripoti katika fomu zake za matumizi ya fedha, jarida la ProPublica imeripoti.

Katika habari ndefu iliyochapishwa Alhamisi, taasisi isiyo ya kiserikali inayofanya habari za uchunguzi imeonyesha safari kadhaa mbalimbali alizofanya Thomas nje ya nchi katika boti ya Crows na ndege nyingine binafsi pamoja na hoteli binafsi za Crows huko Adirondacks. Safari yake ya 2019 kwenda Indonesia habari hiyo imeeleza kwa kirefu ingeweza kumgharimu zaidi ya dola za Marekani 500,000 kama Thomas angekodisha ndege na boti, ProPublica limeripoti.

Majaji wa Mahakama ya Juu, kama majaji wengine wa serikali kuu, wanatakiwa kutoa taarifa ya fedha walizonazo kila mwaka ambapo wanatakiwa kuorodhesha zawadi wanazopokea.

Haikuweza kujulikana kwa nini Thomas aliacha kutoa taarifa ya safari hizo, lakini chini ya muongozo wa sera ya mahakama ambayo Shirika la Habari la AP lilitaka ushauri, chakula, malazi au burudani zinazopokewa kama “ufadhili binafsi kwa mtu yeyote” havihitajiki kuripotiwa iwapo vinafanyika katika nyumba binafsi ya mfadhili huyo au ya familia yake.

Ikiwa ni hivyo, tofauti pekee katika kuripoti haitakiwi kuhusisha “usafiri ambao ni mbadala kwa usafiri wa kibiashara” na mali zinazomilikiwa na mfadhili huyo.

Msemaji wa Mahakama ya Juu alikiri kupokea barua pepe kutoka AP ikitaka maoni kutoka kwa Thomas lakini haikutoa maelezo yoyote ya ziada. ProPublica imeandika kuwa Thomas hakujibu maswali yaliyotaka ufafanuzi kutoka katika taasisi hiyo.

Mwezi uliopita, mahakama ya serikali kuu iliongeza mahitaji ya kutoa taarifa kwa majaji wote, ikiwemo majaji wa mahakama kuu, ingawaje kufikia katika nyumba binafsi za watu kwa ajili ya likizo zinazomilikiwa na marafiki zimeondolewa katika amri hiyo ya kutoa taarifa.

Mwaka jana, masuala mengi kuhusu maadili ya Thomas yaliibuka wakati ilipobainika kuwa hakujiondoa kutoka katika kesi za uchaguzi kufuatia uchaguzi wa 2020 licha ya kuwa mkewe, mwanaharakati wa kiconservative Virginia Thomas, alikuwa akiwasiliana na wabunge na White House kuwasihi wakatae matokeo ya uchaguzi.

Habari hii ya hivi sasa kuna uwezekano ikaongeza shinikizo kwa majaji kufuata utaratibu wa maadili na kuimarisha kuweka wazi safari na zawadi nyingine mbalimbali wanazopokea.

Katika taarifa yake, Crow imeiambia ProPublica kuwa yeye na mkewe wamekuwa marafiki wa Thomas na mkewe tangu mwaka 1996, miaka mitano baada ya Thomas kujiunga na makahama kuu.

Crow alisema “ukarimu wao kwa familia ya kina Thomas kwa miaka kadhaa hauna tofauti na ukarimu ambao tumefanya kwa marafiki wengine wa karibu” na kuwa familia hiyo “haijawahi kuomba ufadhili tuliowafanyia.”

Alisema wao “hawajawahi kabisa kuuliza kesi iliyokuwa haijamalizika au katika mahakama ya chini, na Jaji Thomas hajawahi kujadili kesi yoyote, na sisi hatujawahi kumshawishi Jaji Thomas juu ya masuala yoyote ya kisheria au kisiasa.”

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG