Hatua ya ni ya mwisho kisheria kwa Najib kujaribu kujiondolea lawama ingawa ameomba msamaha kwa serikali ambao kama utakubaliwa, basi huenda akaachiliwa bila kukamilisha kifungo chake cha miaka12 jela.
Masaibu ya Najib yalianza pale ilipogundulika kwamba dola bilioni 4.5 zilikuwa zimeibwa kutoka kwenye mfuko wa 1MDB katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, wakati zaidi ya bilioni moja zikiwekwa kwenye akaunti zinazohusishwa naye.
Mwaka 2021 mahakama ilimkuta na hatia ya kuvunja uaminifu pamoja na ubadhirifu wa fedha kwa kupokea kinyume cha sheria dola milioni 10 kutoka kampuni ya SRC International ambayo ni sehemu ya mpango wa 1MDB.