Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:38

Rais wa Israeli asema hatua ya serikali ya Netanyahu inatishia usalama wa taifa


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, kushoto, na Rais Isaac Herzog baada ya kumpa jukumu Netanyahu la kuunda serikali, huko Jerusalem, Nov. 13, 2022.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, kushoto, na Rais Isaac Herzog baada ya kumpa jukumu Netanyahu la kuunda serikali, huko Jerusalem, Nov. 13, 2022.

Rais wa Israeli Isaac Herzog Jumatatu amemtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuachana na mpango wa kufanya mabadiliko katika mfumo wa mahakama nchini humo, wakati chama kikubwa kabisa cha wafanyakazi kiligoma kupinga mapendekezo ya mabadiliko hayo.

Herzog alitweet kuwa usalama, uchumi na jamii ya Israeli wote wametishiwa, na kwa ajili ya umoja ameitaka serikali “kusitisha mara moja mchakato wa kibunge.”

Amewasihi wabunge kutoka muungano wa utawala na vyama vya upinzani kuwaweka mbele raia wa Israeli juu ya kila kitu, akisema huu ni wakati wa uongozi na uwajibikaji.

Zaidi ya kikundi cha chama cha wafanyakazi wa biashara cha Histadrut kuingia katika mgomo, chama kikuu cha madaktari pia kimetangaza kugoma kupinga mpango huo wa mabadiliko ya mfumo wa mahakama na ndege zilizokuwa zinafanya safari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo zimesitisha safari zake.

Hatua hizo zilizochukuliwa Jumatatu zimefuatiwa na maandamano yaliyofanywa na maelfu ya watu katika maeneo mbalimbali nchi nzima kupaza sauti zao kupinga uamuzi wa Netanyahu kumfukuza kazi waziri wake wa ulinzi.

Waziri Yoav Galant, alielezea upinzani wake kwa mipango ya serikali kufanya mabadiliko kwa mfumo wa mahakama, ikiwemo kuweka amri ya kiutendaji katika uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Juu na kuiruhusu serikali kubatilisha maamuzi ya mahakama kwa idadi ndogo ya waliowengi.

Galant alionya katika taarifa yake iliyotangazwa na televisheni Jumamosi kuwa mgawanyiko juu ya masuala haya “yanapenya katika idara za kijeshi na kiusalama,” yakiwakilisha tishio la kiuslama kwa nchi hiyo.

Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG