Picha za televisheni za shirika la habari la Reuters zimeonyesha umati mkubwa wa watu wakifunga barabara kuu ya mjini Tel-Aviv, na hali kadhalika kundi la waandamanaji wakiwasha moto katikati ya barabara kuu.
Netanyahu amemfukuza kazi waziri wa ulinzi Yoav Gallant siku moja baada ya waziri huyo kujitenga na serikali na kuitaka kusitisha mpango unaopingwa vikali wa kurekebisha mfumo wa mahakama.
Muswada huo na mingine ambayo itapunguza mamlaka ya Mahakama ya juu kuchukua maamuzi dhidi ya sera za serikali, umepelekea shutuma ndani na nje ya nchi juu ya hali ya kidemokrasia ya Israel.
Gallant Jumamosi alikuwa afisa wa ngazi ya juu wa chama cha Netanyahu chenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia kusema kuwa hataunga mkono marekebisho ya mfumo wa mahakama, akisema maandamano yanayojumuisha idadi kubwa ya wanajeshi wa akiba yanaathiri pia wanajeshi wa kawaida na kudhoofisha usalama wa taifa.