Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:29

Mamlaka ya Anga Dubai yasimamisha kwa muda safari za ndege kutoka Kenya


FILE PHOTO: Ndege za Emirates zikionekana uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai nchini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu Januari 13, 2021. REUTERS/Abdel Hadi Ramahi/File Photo
FILE PHOTO: Ndege za Emirates zikionekana uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai nchini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu Januari 13, 2021. REUTERS/Abdel Hadi Ramahi/File Photo

Mamlaka ya Anga ya Dubai imesimamisha kwa muda huduma zote za safari za ndege kwa wasafiri wanaoingia na wanaopitia nchi hiyo kutoka Kenya kwa saa 48 kuanzia Jumatatu saa nne na nusu asubuhi kwa saa za Dubai.

Katika maagizo yaliyotolewa Jumatatu, DCAA imesema wateja hawataruhusiwa kusafiri na ndege ya shirika la Emirates mjini Nairobi wakati huu.

Wasafiri wanaotokea Dubai kwenda Nairobi hawajaathiriwa na uamuzi huu.

DCAA haijatoa maelezo zaidi kwa nini imeahirisha safari za ndege ingawa kumekuwa na wasiwasi juu ya wateja kutoa vyeti bandia vya COVID 19.

Decemba 17 Emirates iliahirisha ndege zake zote kati ya Nigeria na Dubai ikijibu uamuzi kama huo uliofanywa na maafisa wa Nigeria ikipunguza safari za ndege kuwa ndege moja tu kwa wiki.

Wiki iliyopita Kenya imethibitisha kesi ya kwanza ya maambukizi ya kirusi cha Omicron ambapo Wizara ya Afya ya Kenya Jumamosi litangaza kesi za COVID-19 zimeongezeka kuvuka 2,000.

XS
SM
MD
LG