Majeshi ya Somaliland yalipambana na wanamgambo wa kieneo katika mji wa Las’anod siku ya Jumamosi. Kwa kiasi cha siku 50, pande hizo mbili zimejihusisha katika mapigano ambayo yameua zaidi ya watu 200 na kuwajeruhi wenye zaidi ya 600.
Koo za huko Las’anod zimetaka utawala wa serikali kuu huko Mogadishu, lakini Somaliland ilisisitiza kuwa eneo hilo liko chini ya udhibiti wake.
Serikali ya Marekani ilisema Alhamisi kwamba Somaliland ni vyema iondoe majeshi yake kutoka Las’anod ili kufungua njia kwa majadiliano na suluhisho kwa mzozo huo. Hata hivyo, katika maelezo yake Somaliland ilisema kuwa serikali ya Marekani halijalishinikiza serikali ya Puntland kuacha mtiririko wa wapiganaji kwenda huko Las’anod.
Vyombo vya habari vya ndani na watumiaji wa mitandao ya kijamii wamebandika picha Jumamosi ambazo zilimuonyesha mbunge wa zamani wa Puntland Farah Mohamed Dalmar akiwa chini ya ulinzi wa Somaliland baada ya kukamatwa. Dalmar alijiuzulu kama mbunge mwezi Januari na kuripotiwa kujiunga na wanamgambo wa koo wa Las’anod.
Ijumaa, majeshi ya Somaliland waliushambulia mji huo huku kukiwa na ripoti kwamba watu wengi waliuawa. Hiyo ilifuatiwa na taarifa Jumatatu iliyotolewa na jeshi la Somaliland kwamba huenda likaanzisha mashambulizi ili kuchukua udhibiti wa Las’anod.