Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:12

38 wauwawa, na 130 wajeruhiwa Somaliland


Rais wa Somaliland, Muse Bihi Abdi
Rais wa Somaliland, Muse Bihi Abdi

Takriban watu 38 wameuwawa, na zaidi ya 130 wengine wamejeruhiwa kufuatia mapigano ya siku mbili katika mji wa Las Anod, mashariki mwa Somaliland. 

Maafisa wa afya pia wameripoti hospitali ya kuu ya Las Anod, ambayo ni kumbwa katika mji huo pia ilishambuliwa na maguruneti.

Ahmed Mohamed Hassan mkurugenzi wa hospitali hiyo amesema walishambuliwa kwa risasi na kuharibu baadhi ya sehemu za ofisi zao.

Hassan amesema hospitali hiyo ililengwa Jumatatu na Jumanne na baadhi ya wafanyakazi na wagonjwa walikimbia na kwenda kutafuta usalama kwa sehemu nyingine.

Hassan amesema hospitali nyingine zimerekodi vifo, lakini hakutoa idadi ya ziada kwa sababu hakuna mawasiliano na vituo hivyo vingine vya afya.

Somaliland ilitangaza kujitenga na Somalia Mei 1991, lakini bado haijatambuliwa kimataifa. Licha ya kutotambuliwa, Somaliland kwa kiwango kikubwa imesifiwa na jumuiya ya kimataifa kwa kuwepo na uthabiti na kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.

Mapigano baina vikosi vya Somaliland, na wapiganaji wa huko yametokea baada ya kuwepo wasiwasi kwa wiki kadhaa kufuatia kuuwawa kwa risasi mwanasiasa kulikofanywa na watu waliojifunika uso.

Ilikuwa ni shambulizi jipya kabisa katika mfululizo wa mauaji katika eneo hilo kwa miaka mingi, matukio ambayo serekali inawashutumu wapiganaji wa Al-Shabab.

Rais wa Somaliland, Muse Bihi Abdi amewashutumu maadui wa Somaliland kuhusika na mauaji hayo.

Mapigano ya sasa pia yametokea katikati ya mgogoro kuhusiana na hali ijayo ya himaya ya mashariki ya Somaliland, ambapo idadi kubwa ya wakazi wanaunga mkono kuungana na Somalia.

XS
SM
MD
LG