Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:55

Watu 20 wameuwawa Somaliland


Takriban watu 20 wameuawa katika mkoa uliojitenga nchini Somalia wa Somaliland.

Mauaji hayo yametokea katika mapigano kati ya waandamanaji wanaoipinga serikali na vikosi vya usalama kwa siku kadhaa, kulingana na daktari wa hospitali ya serekali.

Kwa zaidi ya wiki moja polisi na wanajeshi wamekuwa wakipambana na waandamanaji huko Laascaanood, mji ulioko mashariki mwa Somaliland wenye mgogoro baina ya Somaliland na eneo la Somalia la Puntland, lenye mamlaka kiasi.

Mohamed Farah, daktari katika Hospitali ya Laascaanood, ameiambia Reuters kwamba takriban watu 20 wameuawa na kadhaa kujeruhiwa.

Waandamanaji wanaitaka Somaliland kukabidhi udhibiti wa mji huo kwa Puntland na pia wanavishutumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kumaliza ukosefu wa usalama mjini humo.

Polisi hawakujibu mara moja simu kutoka kwa Reuters kutoa maoni yao.

XS
SM
MD
LG