Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:00

Utawala wa Somaliland wakubali kusitisha mapigano bila masharti


Washiriki katika mkutano wa Somalia na Somaliland mjini London.
Washiriki katika mkutano wa Somalia na Somaliland mjini London.

Utawala wa mkoa uliojitenga kutoka Somalia wa Somaliland ulisema Ijumaa jioni kuwa umekubali kusitisha mapigano bila masharti, kufuatia siku tano za mapigano mashariki mwa eneo hilo ambalo wahudumu wa afya wanasema yameua darzeni ya watu.

Mapigano makali yalizuka kati ya vikosi vya Somaliland na wanamgambo ndani na kuzunguka mji wa Las Anod, kituo cha utawala cha mkoa wa Sool siku ya Jumatatu baada ya viongozi wa eneo hilo kusema wanataka kujiunga tena na shirikisho la Somalia.

Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka Somalia mwaka 1991 lakini haijapata kutambuliwa kimataifa kwa hadhi yake, na imekabiliwa na upinzani kutoka kwa baadhi ya wazee wa koo katika maeneo yenye migogoro kwenye mpaka wake na jimbo la Puntland lenye uhuru kiasi la Somalia.

“Serikali ya Somaliland imekubali kusitisha mapigano bila masharti usiku wa leo licha ya mashambulizi ya hapo awali ya wanamgambo”, waziri wa ulinzi wa Somaliland Abdiqani Mahamoud Ateye aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Haijabainika mara moja ikiwa usitishaji mapigano ulikuwa unazingatiwa katika uwanja wa vita, lakini Abdirizak Mohamed Hassan, msemaji wa kundi linalopinga utawala wa Somaliland, liliita usitishaji huo wa mapigano kuwa ni uongo.

XS
SM
MD
LG