Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 17:32

Majeshi ya Israeli yamuua Mpalestina karibu na eneo takatifu lenye utata mjini Nablus


Waombolezaji wa Kipalestina wamebeba mwili wa Hamza Maqbool, 32, ulioko nyuma na Khayri Shaheen, 34, wakati wa maziko yao katika eneo la mji wa Nablus ulioko Ukingo wa Magharibi, Ijumaa, July 7, 2023.
Waombolezaji wa Kipalestina wamebeba mwili wa Hamza Maqbool, 32, ulioko nyuma na Khayri Shaheen, 34, wakati wa maziko yao katika eneo la mji wa Nablus ulioko Ukingo wa Magharibi, Ijumaa, July 7, 2023.

Majeshi ya Israeli yamemuua Mpalestina mapema Alhamisi karibu na eneo takatifu lenye utata katika mji wa Nablus ulioko Ukingo wa Magharibi, unaokaliwa kimabavu na Israeli, wizara ya afya ya Palestina ilisema.

“Raia mmoja aliuawa kwa risasi za wavamizi (Waisraeli) katika mji wa Nablus,” taarifa kutoka wizara hiyo ilisema, bila ya kufafanua utambulisho wa marehemu huyo na kuongeza kuwa watu wengine watatu waliojeruhiwa walifikishwa hospitali.

Jeshi hilo la Israeli halikutoa tamko mara moja kuhusu tukio hilo.

Tukio hilo limejiri katikati ya mvutano unaoongezeka huko Ukingo wa Magharibi, kufuatia mashambulizi kadhaa ya Wapalestina kwa walowezi wa Israeli, na ghasia za walowezi wa Israeli dhidi ya Wapalestina.

Gari la jeshi la Israeli lilishambuliwa katika mapambano na Wapalestina wakati jeshi la Israeli lilipovamia mji wa zamani wa Nablus katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israeli huko Ukingo wa Magharibi Julai 7, 2023.Photo by Jaafar ASHTIYEH / AFP)
Gari la jeshi la Israeli lilishambuliwa katika mapambano na Wapalestina wakati jeshi la Israeli lilipovamia mji wa zamani wa Nablus katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israeli huko Ukingo wa Magharibi Julai 7, 2023.Photo by Jaafar ASHTIYEH / AFP)

Walioshuhudia tukio hilo wameiambia AFP kuwa jeshi hilo lilikuwa linasindikiza kikundi cha Waisraeli kuelekea eneo la ibada karibu na Nablus ambapo darzeni ya Wapalestina walichoma moto matairi na kuwarushia wanajeshi vilipuzi na mawe.

Waisraeli hao walikuwa wanaelekea katika Kaburi la Joseph, likisadikiwa kuwa ni sehemu ya mwisho ya mapumziko ya kiongozi wa kidini Joseph, eneo ambalo linaghasia za mara kwa mara katika Ukingo wa Magharibi, na linatukuzwa kama eneo takatifu.

Jeshi hilo mara kwa mara linawasindikiza mahujaji kufika katika eneo hilo, wakati Wapalestina wanadai ziara hizo ni uchokozi.

Ghasia zinazohusishwa na mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina mwaka huu zimeuwa Wapalestina wasiopungua 196, Waisraeli 27, raia wa Ukraine moja na wa Italia mmoja, kulingana na hesabu iliyojumuishwa na Shirika la Habari la AFP kutoka vyanzo rasmi vya pande zote.

Inajumuisha, upande wa Wapalestina, wapiganaji na raia, na upande wa Israeli, zaidi raia na wanajumuiya watatu wa Waarabu waliowachache.

Israeli imeikalia kimabavu Ukingo wa Magharibi tangu mwaka 1967. Takriban Waisraeli 490,000 wanaishi katika eneo la makazi yanayochukuliwa ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG