Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:12

Israeli kununua ndege za kivita za F-35 kutoka Marekani


Ndege aina ya kivita ya F-35.
Ndege aina ya kivita ya F-35.

Israeli itanunua ndege 25 za F-35 kutoka Marekani, Wizara ya Ulinzi ya Israeli ilitangaza Jumapili, katika makubaliano ambayo yataongeza idadi ya ndege za kivita za jeshi la nchi hiyo, kwa asili mia 50.

F-35 ndiyo ndege ya kivita ya hali ya juu zaidi duniani, na Israeli ndiyo nchi pekee katika Mashariki ya Kati inayozimiliki.

Israeli itanunua ndege 25 za F-35 kutoka Marekani, Wizara ya Ulinzi ya Israeli ilitangaza Jumapili, katika makubaliano ambayo yataongeza idadi ya ndege za kivita za jeshi la nchi hiyo, kwa asili mia 50.F-35 ndiyo ndege ya kivita ya hali ya juu zaidi duniani, na Israeli ndiyo nchi pekee katika Mashariki ya Kati inayozimiliki.

Ununuzi huo wa dola bilioni 3, ambao unaongeza ndege za F-35 za Israeli kutoka 50 hadi 75, unatarajiwa kukamilishwa katika miezi ijayo, wizara hiyo ilisema.

Ilisema mpango huo utafadhiliwa kupitia msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Israeli, na kwamba mtengenezaji wa ndege hiyo, Lockheed Martin, na mtengenezaji wa injini yake, Pratt & Whitney, wamejitolea kuhusisha makampuni ya Israeli katika mchakato wa uzalishaji wa vyombo hivyo.

"Makubaliano hayo mapya yatahakikisha kuendelea kwa ushirikiano kati ya makampuni ya Marekani na viwanda vya ulinzi vya Israeli katika utengenezaji wa vifaa vya ndege," ilisema taarifa hiyo.

Hatua ya kuongeza silaha za Israeli imekuja wakati ambapo mvutano umeongezeka kati ya nchi hiyo na Iran. Israeli, ambayo inaichukulia Iran kuwa hasimu wake mkuu, hapo awali iliwahi kutumia ndege za F-35 kutungua ndege zisizo na rubani za Iran, na imetishia kufanya mashambulizi ya masafa marefu, yakilenga vinu vya nyuklia vya Iran.

Forum

XS
SM
MD
LG