Wakiwa wamevalia mavazi meusi na yenye kuwaficha, wanachama wa Brigedi ya Ezzedine al-Qassam walitangamana na vijana wa kiume na wa kike kwenye maonyesho hayo katika uwanja unaoitwa Unknown Solider’s Square huko Gaza.
Kundi hilo lilitoa mwaliko kupitia mitandao ya kijamii na mabango misikitini na kusema wajumuike kuona na kupiga picha na silaha za Al-Qassam.
Tukio hilo lilikuwa la kwanza ambapo Hamas imeuruhusu umma kupiga picha na silaha.
Tukio hilo linafanyika baada ya kuongezeka kwa ghasia za hivi karibuni kati ya Israel na Palestina, ambazo ziligharimu maisha ya Wapalestina 16 na Waisraeli wanne huko Ukingo wa Magharibi, mwishoni mwa Juni.
Mwezi Mei, makundi ya wanamgambo wa Gaza na Israel yalifanya mapigano ya kuvuka mpaka kwa muda wa siku tano, na kuwauwa Wapalestina 34, miongoni mwao wakiwa makamanda sita wa Islamic Jihad, wapiganaji kutoka makundi mengine yenye silaha ya Palestina na raia wa kawaida wakiwemo watoto.
Forum