Jeshi lilitangaza kuhusu shambulizi hilo baada ya Mpalestina mmoja kuuawa mapema Jumatano, katika kijiji kinachokaliwa kwa mabavu cha Ukingo wa Magharibi, kilichoshambuliwa na mamia ya Waisraeli.
Taarifa za kijasusi zilipelekea wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kutambua kundi hilo "ndani ya gari lililotiliwa shaka, baada ya magaidi hao kuanza kufyatua risasi karibu na mji wa Jalamah", ulio karibu na Jenin kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, taarifa ya jeshi ilisema.
Shambulizi hilo ni la kwanza kufanywa na Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi tangu mwezi Agosti mwaka 2006, chanzo cha kijasusi cha Palestina kililiambia shirika la habari la AFP. Hata hivyo, hapo awali, chanzo hicho kilisema ni shambulizi la kwanza tangu mwaka 2005, kabla ya kuripoti kuwa wanamgambo wawili waliuawa katika shambulizi la mwaka 2006.
Awali, wakazi wa mji wa Turmus Ayya walisema idadi ya walowezi wa Kiisraeli waliohusika katika shambulio la kijiji chao, ikuwa kati ya 200 na 300, wakati waandishi wa habari wa AFP wakiripoti kushudia nyumba zilizochomeka, majengo yaliyoharibiwa, na watu waliojeruhiwa, wakiondolewa kwa gari la wagonjwa.
Forum