Mipango ya serikali ya kurekebisha mahakama iliitumbukiza Israel katika moja ya migogoro mibaya zaidi ya nchi hiyo kuwahi kutokea mapema mwaka huu.
Mazungumzo kati ya serikali na vyama vya upinzani kwa kiasi fulani yalipunguza mzozo huo kwa majaribio ya kutafuta msingi wa mapendekezo ya mabadiliko ya mahakama.
Mazungumzo hayo yalivunjika wiki iliyopita kutokana na mzozo unaozingira kamati yenye nguvu inayohusika na kuchagua majaji wa nchi hiyo.
Viongozi wa upinzani wamesema mazungumzo yalisitishwa hadi kamati hiyo itakapoundwa.
Katika mkutano wa Baraza lake la Mawaziri siku Jumapili, Netanyahu alisema upinzani haujafanya mazungumzo kwa nia njema na kwamba serikali yake itaendelea kwa tahadhari katika urekebishaji huo.
Forum