Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu iliendeleza hatua hiyo yenye utata licha ya maandamano makubwa tangu kupendekezwa kwa mageuzi hayo mwezi Januari.
Waandamanaji walifunga barabara katika maeneo mbalimbali nchini humo, na kukusanyika katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion karibu na Tel Aviv, huku polisi wakiripoti kukamatwa kwa watu 42 kote nchini kufikia saa tano asubuhi, saa za huko.
Polisi katika taarifa walisema "wanaidhinisha uhuru wa kuandamana huku wakizingatia sheria na utulivu". Viongozi wa waandamanaji walikuwa wametangaza Jumanne, kama siku ya kuhamasisha wananchi, huku wakisubiri kura ya bunge, huku darzeni ya mikutano ya hadhara ikitarajiwa kote nchini.
Maandamano yalikuwa yamepangwa kufanyikamjini Tel Aviv nje ya ubalozi wa mshirika mkuu wa Israeli, Marekani. Katika mahojiano na shirika la habari la CNN yaliyopeperushwa Jumapili, Rais wa Marekani Joe Biden alisema anatumai kwamba Netanyahu "ataendelea kuelekea kwenye usawa na mabadiliko katika mahakama."
Forum