Shambulizi hilo limetokea chini ya wiki moja baada ya zaidi ya watu 200 kuuawa katika jimbo la Zamfara, kaskazini magahribi mwa Nigeria.
Watu 18 wameuawa katika shambulizi dhidi ya jamii ya Ncha, katika sehemu ya Bassa, jimbo la Plateau, huku wwatu wengine 34 wakiuawa katika sehemu za Nakuna na Wurukuchi, jimbo la Niger.
Tukio katika jimbo la Niger limeonekana kuwa la kulipiza kisasi, baada ya kutokea mauaji wiki chache zilizopita pale wawindani maalum na wapiganaji wa kijamii katika sehemu hiyo kuua watu kadhaa waliokuwa wamejihami kwa silaha na waliokuwa wanashutumiwa kwa kuwahangaisha watu katika jamii.
Watu wenye bunduki walianzsiaha mashambulizi dhidi ya jamii za Nakuna na Wurukuchi walipokuwa wakivuna mazao shambani. Nyumba kadhaa zilichomwa moto katika sehemu ya Nakuna.
Mkuu wa polisi katika jimbo la Niger Monday Kuryas, amethibitisha tukio hilo lakini amesema hana idadi kamili ya watu waliouawa kufikia wakati tulikuwa tunaandaa ripoti hii.