Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 25, 2024 Local time: 04:16

Mahakama yatupilia mbali madai ya mashirika ya haki za binadamu juu ya vipuli vinavyoweza kutumika Gaza


Ndege za kivita aina ya F-35
Ndege za kivita aina ya F-35

Mahakama moja nchini Uholanzi siku ya Ijumaa imetupilia mbali madai ya kikundi cha mashirika ya haki za binadamu yakidai kuwa Uholanzi inakwepa amri ya mahakama kusitisha kupeleka  vipuli vya ndege za kivita F-35 kwa Israel ambavyo wanaweza  kuvitumia huko Gaza.

Mahakama ya Wilaya ya The Hague imetoa uamuzi kuwa Oxfam Novib, Pax Nederland na Taasisi ya The Rights Forum zilikuwa hazijaonyesha ushahidi wowote kuwa serikali ya Uholanzi ilikuwa inapuuza uamuzi huo wa awali wa mahakama.

Mwezi Februari, mahakama ya rufaa iliiambia serikali ya Uholanzi kusitisha usafirishaji wa vipuli vya ndege za kivita F-35 kwenda Israel, ikielezea kuwa kuna hatari ya kukiukwa sheria za kimataifa iwapo vitatumika kufanya mashambulizi Gaza. Serikali ya Uholanzi ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika Mahakama ya Juu, lakini ilisema ilikuwa inaheshimu amri iliyotolewa wakati huu kwa kusitisha kusafirisha moja kwa moja vipuli hivyo Israel.

Vikundi vya misaada vilirejea tena mahakamani mwezi uliopita, vikitoa hoja ya kuwa Uholanzi ilikuwa inakiuka katazo la kupelekea vipuli hivyo Marekani, ambayo ilikuwa hatimaye inavipeleka Israel. Wametaka watozwe faini kwa madai hayo ya kuvunja sheria.

Vikundi hivyo “vinatoa tafsiri pana mno” kwa uamuzi huo wa mahakama, mahakama hiyo iliandika katika uamuzi wake.

Mashirika hayo yalisema hawakubaliani na uamuzi huo na wanatafakari kuchukua hatua zaidi za kisheria.

“Haikubaliki kwa Uholanzi inabaki ikifahamu inashiriki kuona kuwa sheria za vita zinavunjwa na Israel huko Gaza,” walisema katika taarifa yao ya pamoja.

Wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo mwezi Juni, serikali ya Uholanzi ilisema haiwezi kufuatilia vipuli hivyo vinapoondoka Uholanzi na kuonya juu ya kuwekewa vikwazo zaidi.

F-16 fighter jet ikiwa katika hema la matengenezo South Burlington, Vermont, Marekani Dec. 17, 2012.
F-16 fighter jet ikiwa katika hema la matengenezo South Burlington, Vermont, Marekani Dec. 17, 2012.

Reimer Veldhuis, wakili anayeiwakilisha serikali, alitahadharisha kuwa kutaka kuzuia usafirishaji zaidi wa vipuli vya F-35 kwa mataifa mengine na siyo Israeli inaweza kuyaweka hatarini majeshi mbalimbali duniani ambayo yanatumia ndege hizo za kisasa za kivita wakati ambapo kuna ongezekola mivutano ya kimataifa.

Uholanzi ni makao makuu ya moja ya ghala tatu za Ulaya za F-35.

Vita hiyo ilianza Oktoba 7 wakati wapiganaji wa Hamas wakipofanya shambulizi la kushtukiza kwa Israel hapo Oktoba 7, ambapo wanamgambo waliwaua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka wengine 250.

Tangu wakati huo, mashambulizi ya ardhini ya Israel na ya mabomu huko Gaza yameua zaidi ya watu 38,000 huko Gaza, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya eneo hilo, ambalo halijatofautisha kati wapiganaji na raia katika hesabu yao.

Forum

XS
SM
MD
LG